Monday, January 23, 2017

Taarifa kwa umma

TAARIFA KWA UMMA



MABALIKO YA NJIA YA DALADALA KITUO CHA GEREZANI KWA SIKU YA TAREHE 25 JANUARI 2017



Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) inawafahamisha abiria, wamiliki, madereva wa daladala na umma kwa ujumla kuwa:

·        Siku ya Jumatano tarehe 25 Januari 2017 kuanzia asubuhi hadi saa tisa alasiri kutakuwa na mabadiliko ya njia ya daladala katika kituo cha Gerezani kilichopo eneo la Kariakoo.

·        Hii ni kwa ajili ya kupisha shughuli ya uzinduzi waMiundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka  utakaofanyika siku hiyo kwenye kituo hicho.

·        Aidha kwa siku hiyo, daladala zote ambazo huishia kituo cha Gerezani zitapaswa kuishia vituo mmbadala vyaMachinga Complex na Gerezani ‘Railway Club’ kwa utaratibu ufuatao:

·        Daladala zinazotumia  Barabara ya Nyerere  na  Chang’ombe  siku hiyo zitapita Barabara ya Kawawa - Lindi hadi Machinga Complex  nakurudi kwa kutumia  Barabara ya Kawawa

·        Daladala zinazotumia  barabara ya Kilwa siku hiyo  zitaishia eneo ilipokuwa  ‘Railway Club’ na kurudi zilipotokea.

·        MUHIMU: Magari yanayoelekea Kituo cha Mnazi Mmoja yataendelea kwenda Mnazi Mmoja bila kuathirika na utaratibu huu.

·        SUMATRA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza



SUMATRA kwa usafiri bora na salama!

Imetolewa na:

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini  (SUMATRA)

(Tafadhali wasambazie wengine wapate taarifa)

No comments:

Post a Comment