Monday, January 30, 2017

HEBU FANYA HAYA UFURAHIE NDOA YAKO


HEBU FANYA HAYA UFURAHIE NDOA YAKO


1. MAPOKEZI

Anaporudi kutoka kazini, safarini au kwenye shughuli yake yoyote ile, anza kwa salamu nzuri. Mpokee na kumkumbatia huku uso ukiwa na tabasamu la bashasha.
2. MAVAZI

Jipambe na upake manukato kwa ajili yake mpenzi wako. Vaa vizuri nguo ziwe za kuvutia na za kumtega mnapokua chumbani.

3. USAFI WA MWILI.

Ili kumteka akili mumeo inatakiwa ujue kuoga vizuri na ujue kuzisafisha sehemu nyeti  vizuri na ikiwezekana ipake misk au ifukize udi,japo si shauri Sana matumizi ya miski sehemu nyeti

4. JUA NAMNA YA KUZUNGUMZA NA MUMEO

Unapoanza kuzungumza naye anza na mambo au taarifa nzuri, na kama kuna taarifa mbaya subiri mpaka ale apumzike ndio umuambie.

5. SAUTI

Pendezeshe na uilainishe sauti yako kwa ajili ya mumeo,kwani sauti ni silaha muhimu  huongeza nakshi katika masikio yake… usifanye hivyo mbele ya wanaume wengine ni haramu .

6. MTINDO

Jitahidi mara kwa mara kubadili mtindo wa nywele, manukato na kadhalika.

Lakini usizidishe kiwango na ufanye hivyo kwa mumeo tu.

7. MAHANJUMATI

Mpikie chakula kitamu ajirambe maana waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea.
Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi huwa wanajali ladha tu.

Mpe mapishi matamu ili kumfanya akumiss pale anapokosa huduma yako.

8. SHUKURU

Kuwa mwenye shukrani kwa mumeo Kwa kikubwa na kidogo.  Ukiwa mwenye shukrani, mumeo atazidi kukupenda na atajitahidi kukufurahisha na kukuridhisha zaidi.

Ukiwa mtovu wa shukrani, mumeo atasikitishwa na hali hiyo na kuanza kujiuliza: “Kwa nini nimfanye mambo mazuri mtu asiyekuwa na shukrani?” Epuka Sana hali hiyo.

9. HESHIMA NA UTIIFU

Daima kuwa mtiifu kwa mumeo pia uwe mwaminifu kwa kipenzi chako.

10. Muunge mkono kupitia kazi yake, fedha yake au mali yake pindi inapohitajika. Japo hii wanawake wengi hushindwa kufanya hivyo.

11. MAAGIZO.

Fuata maagizo yake kama kufanya ibada, stara, ukarimu, nidhamu no. isipokuwa katika mambo ya haramu katika Uislamu.

mume ni kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na ni mshauri wake.

12. EPUKA

Jaribu kuepuka yale yanayomkasirisha mumeo

Mfurahishe anapokuwa ameghadhibika.

13. OMBA RADHI

Ukimkosea mumeo muombe msamaha. Na akikosea usihamaki kwa kumfokea au kuzozana naye.

Subiri anapokuwa hana ghadhabu na uzungumze naye kwa amani na kwa kauli nzuri.

14. MAPENZI MATAMU


Mpe mapenzi motomoto kwa style mbalimbali usiwe na style moja , usichelewe kumpa mahaba pindi mumeo anapojiwa na hisia ya kutaka kufanya mapenzi.

Mwambie maneno mataamu na yenye mvuto wa kimahaba.

15. MSIFIE MUMEO

Jua kumsifia babydady kwa zuri atakalokufanyia sio unakaa kimya.

16. ENJOY NAYE.

Mtoe out babydady siku moja moja na siku nyingine, pendelea kutumia muda mwingi kuongea nae maneno mazuri mkiwa wote nyumbani/chumbani.

17. MASSAGE.

Mfanyie massage ya mwili na sehemu nyeti mumeo, vilevile msinge mmeo anapokua nyumbani siku za weekend tumia muda mwingi kumfanyia hayo mambo.

18. MAJINA MATAMU.

Mwite mpenzi wako majina mazuri ya kimapenzi , haiji kumwita mumeo baba sikujua? khaaa, ina husu......

Ili kuiteka akili ya mwanaume muite majina mazuri kama honey, dear, sweet, darling, dady ukishindwa mwite jina lake nusu liwekee swagaa flan

 mfano waweza ita my Jey, badala ya jumaa au Bin Rash  wangu badala ya Bin Rashid wangu jitahidi best.

Best hakuna mchawi wa mapenzi ukifanya yote hayo utakua umeteka akili yake na hatobanduka kwako abadani..

No comments:

Post a Comment