Friday, January 27, 2017

BORESHA AFYA YA NYWELE ZAKO KWA KUTUMIA TUI LA NAZI


BORESHA AFYA YA NYWELE ZAKO KWA KUTUMIA TUI LA NAZI


Wanawake wengi wamekuwa wakihangaika katika kuhakikisha kuwa wanatunza nywele zao dhidi ya matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na mba au kukatika kwa nywele jambo ambalo limekuwa likiwagharimu pesa pia.



Wataalam wa tiba za asili  wanasema kuwa njia mojawapo ya kuboresha nywele zako ni kuziosha nywele kwa tui la nazi, ambapo anasema kuwa mara baada ya kuosha nywele zako vizuri, ukachukuwa tui la nazi lililochunjwa vizuri na uoshee nywele zako huku ukihakikisha tui hilo linafika hadi kwenye vishina vya nywele.


Wataalam hao anaendelea kubainisha kuwa tui hilo litakuwa ni tiba nzuri kwa ajili ya tatizo la mba na kuzifanya nywele zako kukua kwa haraka zaidi na kuzifanya zionekane zenye afya tele.


Mbali na mafuta hayo ya nazi, wa taalamu wanashauri, kuwa mbegu za ndimu na pilipili manga zikichanganywa pamoja na kupondwapondwa na kisha kuchanganywa na tangawizi, mchanganyiko huo husaidia sana kuotesha nywele endapo mhusika atapaka kila siku jioni.





Vitu vingine ambavyo vinaweza kurutubisha nywele zako ni pamoja na ndimu, ufuta na mafuta ya nazi



No comments:

Post a Comment