Wakina mama wengi wanakuwa wanajiuliza bila kupata majibu kama ni sahihi kumpa mtoto mchanga maji .Taasisi za afya dunia kama (World health organization) hazishauri mtoto chini ya miezi 6 kunywa maji,sababu tafiti nyingi zimeonyesha kwamba maziwa ya mama au baby formula yanakiasi cha maji ya kutosha kumtosheleza mtoto.
Sababu zinazomfanya mtoto asipewe maji
Maji kuharibu uwezo wa mwili wa mtoto kunyonya virutubisho vya maziwa ya mama ipasavyo.Maji yatamjaza tumbo mtoto kumfanya ashibe na atashindwa kunyonya kwa kiasi kinachotakiwa.Water intoxication-hii ni hali ya mwili kuwa na kiwango kikubwa cha maji na kuadhiri afya ya mtoto anaweza akazimia mara kwa mara na kumpelekea hata kukaa comaMaji sio salama ,mwili wa mtoto bado ni mdogo hauna kinga ya kutosha kupigana bakteria au virus wanao weza patikana kwenye maji.
Mtoto anaweza pewa kiwango kidogo cha maji iwapo
Anaishi eneo lenye joto kali sana ,anaweza pewa vijiko 2-3 vidogo vya chaiMtoto alieanzishiwa kunywa uji mwepesi kabla ya miezi 6 anaweza pewa vijiko 3-4 vya chai mara 2 kwa siku.
Ushauri
afyaborakwamtotoWatoto wanaopewa maziwa ya kopo (baby formula) au maziwa ya mama hawana haja ya kupewa maji mpaka watakapo fikisha miezi 6,mama anaenyonyesha anatakiwa kunywa maji kwa wingi isipungue glasi 7-8 kwa siku.Mama anaweza kuzalisha maziwa machache na ikamfanya mtoto asishibe hivyo anaweza kupika uji mwepesi iwapo mzazi hana uwezo wa kuwanunulia maziwa ya kopo ,mtoto anekunywa uji apewe maji ya kunywa kwa kuzingatia vipimo sahihi vijiko 3-4 mara 2 kwa siku,ili kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
No comments:
Post a Comment