Sunday, February 26, 2017

Jinsi Ya Kutumia Mbinu Ya Utabiri Kumvunja Nguvu Mwanamke Ili Abaki Na Wewe Milele

Jinsi Ya Kutumia Mbinu Ya Utabiri Kumvunja Nguvu Mwanamke Ili Abaki Na Wewe Milele

Ok, hebu tuanze kwa kuuliza maswali. Je ushawahi kuwa na girl friend? Kama huna girlfriend mpaka siku ya leo unangojea nini?
Na kama umekuwa na girlfriend muda huu wote, je wewe na huyu girlfriend wako mnaishi vipi? Je mnazozana, mnakosana, ama hamuelewani?

Katika mahusiano haswa inapotokea kuwa nyote wawili mnapendana lakini kuna mmoja wenu hajaridhika na mwenzake basi mara nyingi ukifanya uchunguzi utakuja kugundua kuwa mmoja kati ya nyinyi wawili huwa ana mchepuko/ mpango wa kando.

Na mara nyingi inauma sana iwapo huyo ambaye anakuwa na mpango wa kando ni mpenzi wako, na mbaya zaidi ni pale ambapo bado unampenda huyu mpenzi wako.

Kwa kueleza kifupi ni kuwa umegundua kuwa mpenzi wako ana mpenzi wa kando na wewe hujaridhika na hio hatua ya yeye kutaka kukuacha na kumfuata huyo mwingine.

Ikifikia hapa utachukua hatua gani ili asikuache? Hapa ndipo hii mbinu ya ‘utabiri’ inaingia kati.

Hebu tuuchukulie huu mfano. Wakati mteja ameingia katika duka flani anataka kununua bidhaa lakini hajaridhishwa na bidhaa anazoziona na anataka kuenda katika duka la pili huwa mhudumu kwa kawaida hamkatizi tamaa yake ya kuenda katika duka la pili bali humpa mawazo na hutabiri kile ambacho atapatana nacho katika duka la pili. Kwa kawaida atamwambia, “Jiskie huru kuenda katika duka flani na flani , lakini kumbuka kuwa maduka hayo huwa bei zao ziko juu kupita kiasi, ama hutapata bidhaa mahususi unayotafuta, ama utadhulumiwa nk.

So, huyu mhudumu amefanya nini hapa? Rahisi! Kama huyu mteja ameshawishika na kuamua kubaki hapo, atakuwa ameshinda. Kama huyu mteja ameamua kuenda katika duka la pili, na kugundua kuwa kile alichoambiwa ni kweli na kurudi tena, atakuwa pia ameshinda. Na kama ataenda na hatarudi, basi hakutakuwa na utofauti wowote kama vile awali.

Sasa hebu fikiria kidogo jinsi ya kuitumia mbinu hii kwa girlfriend wako ama kwa mpenzi wako. Unaweza kutumia hii mbinu kumvunja nguvu iwapo kuna mwanaume flani yeyote pale ambaye anamtatiza kihisia.

Kwa mfano unaweza kumwambia, “Uko huru kuendelea na yeye, ni kawaida, inakubalika. Lakini najua kufikia hadi sasa umeshagundua kuwa huyo unayemfuata ana tabia ambayo si nzuri kwako, tabia ambayo inakutatiza na kukusumbua... na utapata kugundua tabia nyingine mbaya zaidi kadri ambapo utazidi kuendelea kuwa na yeye.”

Hapa moja kwa moja atajaribu kuvuta taswira za tabia zozote mbaya ambazo ashawahi kuzishuhudia kutoka kwa huyu mwanaume.
 Kumbuka utabiri unaoutoa hapa utakuwa hauna uhusiano mmoja kwa moja na huyu mwanaume bali unasema na kubahatisha tu. Lakini kwa mwanamke atadhania kuwa tayari unamjua huyu mwanaume na tabia zake.

So moja kwa moja kama huyu mwanamke kweli ana hisia kwako anaweza kubadili msimamo wake na kukubali kuendelea na wewe.
Upo!?

Thursday, February 16, 2017

HATUA KUMI ZA KUCHAGUA MCHUMBA

HATUA KUMI ZA KUCHAGUA MCHUMBA


Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.

Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.


Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, , viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.


Thursday, February 9, 2017

Jinsi ya kuifanya ngozi yako kuwa na afya na mng'ao kwa kutumia vitu vya asili

Urembo: Jinsi ya kuifanya ngozi yako kuwa na afya na mng'ao kwa kutumia vitu vya asili



Uzuri wa ngozi sio rangi tu bali ni
muonekano wa ngozi yenyewe kwamba ina afya na mng'ao unaoashiria afya njema.
Leo tushirikishane jinsi ya kufanya facial treatment kwa kutumia vitu vya jikoni kama kiini cha yai,machicha ya nazi,tango na limao.Treatment hii inaweza kufanyika Mara moja kwa wiki au kila baada ya wiki mbili, unaweza kufanya hata mara moja kwa mwezi ukipata nafasi kama unakuwa busy sana lkn matokeo mazuri utayashuhudia.

Andaa maji masafi yenye joto kiasi unachomudu ktk ngozi yako, osha uso wako kwa hayo maji safi .
Kama una ngozi kavu au ya kati chukua kipande cha tango kidogo na upake yale maji yake usoni,



 kwa wenye ngozi ya mafuta unaweza kutumia kipande cha limao kwa kupaka maji yake.


Chukua pamba au kitambaa laini na futa maji ya matunda usoni kwa mtindo wa kusafisha taratibu usoni.
Chukua machicha ya nazi na Anza kuusugua uso  na shingoni taratibu Mpaka uridhike uso wote umepitiwa na machicha yako hasa unapoona unang'aa kwa mafuta kidogo yaliyotoka kwenye nazi. Kisha pukuta yale machicha ubaki na uso unaong'aa bila vitu vyeupe yaani machicha.


Chukua kiini cha yai inapendeza ukitumia la kienyeji, au la kisasa lenye kiini cha njano iliyokolea angalau. Ili kiini kisijichanganye na ute wakati wa kupasua ,ligonge yai upande mmoja sio katikati na limimine ktk chombo mithili ya sahani ambayo unaona kiini katikati kisha unakichota na kuweka kando. Paka ule uji mzito wa njano wa kiini uso mzima bila kusahau shingoni na nyuma ya masikio na ngozi ya masikio.


Baada ya kupaka kiini cha yai unaweza kuendelea na shughuli zako huku likiendelea kukauka,linapokauka ngozi yako inakuwa kama inajivuta vuta.Baada ya kule kuvuta kuisha inamaanisha yai limekauka kabisa. Osha uso wako kwa maji safi maji yawe ya baridi sasa.Jinsi inavyofanya kaziTango au limao hutumika kama cleanser, unapokuja kujifuta taratibu unaondoa uchafu katika ngozi yako.Machicha ya nazi yanatumika kama scrub, yanaondoa seli zilizokufa, kuifanya ngozi kuwa laini na kuipa mngao.Kiini cha yai hapa kinatumika kama maski, matundu ya ngozi yanajifunga vizuri na kinaipa ngozi yako lishe kutokana na vitamins zilizomo kwenye kiini cha yai kama vitamin E.Mwishoni unanawa na maji baridi ili kuruhusu matundu ya ngozi kujifunga na kuifanya ngozi ijiweke sawasawa.Faida za hii treatmentHusaidia kutibu na kuikinga ngozi na chunusi,Kuipa ngozi mng'ao bila kutumia kemikali za sumu,Husaidia kupunguza mikunjo ktk ngozi yako(wrinkles zinapungua)Gharama ndogo kuifanya

Wednesday, February 8, 2017

majina 65 yaliyotajwa leo sakata ya madawa ya kulevya

Mbowe,Manji ,Idd Azan,Mch.Gwajima ni  kati ya majina  65 yaliyotajwa leo sakata ya madawa ya kulevya #RC Makondo
MMILIKI WA SLIPWAY...

YATCH CLUB..
MMI SALEH..

MWINYI MACHAPTA

BALOZI
KIBOKO WA MBEZI YA CHIN
ALLY FIDHI MBEZI CHIN

IDDI AZAN

MBOWE

BOSS CHIZENGA

MASANGA,Bunju

Deo mchanga

Mahalifu

Abel mfundo

Kizza

Kitwana

Hashiri

Halidi mwarabu

Nassoro selem

Hussein mwarabu

Hussein pamba kali

Gwajima

Yusuph manji

Mmiliki wa cassino la Sea Cliff..

Petroleum limited

GPB


Monday, February 6, 2017

SIFA KUMI ZA MWANAMKE ANAYEJITAMBUA.....

SIFA KUMI ZA MWANAMKE ANAYEJITAMBUA.....

1. Wanaume huchagua wanawake kama vile mtu anachagua yeboyebo zilizotandazwa chini sokoni na kwa mwanaume yeyote ataokota tu zile ambazo ziko karibu yake wakati mwingine hata kama hazimtoshi. Lakini kwa mwanamke anayejitambua na anayejua thamani yake atakuwa sawa na kiatu kizuri ambacho kimetundikwa dukani juu kabisa tena kwenye duka la kioo ambacho hakipatwi hata na vumbi. Anajua thamani yake hivyo atamfanya mwanaume amhangaikie kumfuata dukani na kumchagua kwa heshima, hata jirahisisha na kuruhusu kutandazwa tandazwa chini.
2. Mwanamke anayejitambua anapaswa kujua kuwa mahusiano yanachangamoto lakini angalau asilimia 8o ya muda wenu muutumie mkifanya mambo yakuwapa furaha, kama mnatumia zaidi ya asilimia ishirini ya muda wenu kugombana basi jua uhusiano wenu hauendi popote, jitathimini kama unamhitaji huyo mtu au la?
3. Mwanamke anayejitambua hujipenda yeye mwenyewe kwanza kabla ya kumpenda mwanaume, hii ni kutokana na ukweli kuwa, kama hujipendi hata kama ukipendwa vipi huwezi furahia upendo huo.
4. Mwanamke anayejitambua anajua pia ni kitu gani anakitaka kwa mwanaume na anahakikisha anakipata. Kama hujui unachokitaka kwake hata ukikipata bado utajihisi hujakamilika, hembu jiulize sasa unataka nini kwenye mahusiano uliyonayo sasa.
5. Mwanamke anayejitambua halinganishi mahusiano yake ya sasa na yazamani, au mahusiano yake na mahusiano ya rafiki yake. Huamua kuwa na furaha sasa bila kujali huko nyuma maisha yalikuwaje, husahau yaliyopita na hahangaishwi na mambo yanayofanywa na wengine.
6. Mwanamke anayejitambua huchagua aina ya mwaname anayemtaka na si kuchukua tu kila mwanaume kwakuwa tu ni mpweke au anahisi umri umeenda.
7. Mwanamke anayejitambua hujitoa kimwili kwa mwanaume pale anapohisi kuwa yuko tayari kufanya hivyo na si kwakuwa anaogopa kumpoteza mwanaume, kwani anajua thamani yake na anajua kama mwanaume anamthamini basi hatajali sana kuhusu ngono bali ataangalia upendo wa kweli.
8. Mwanamke anayejitambua anafahamu kuwa mwanaume si Baba yake, Kaka yake au Bosi wake bali ni rafiki yake, hivyo atamheshimu lakini hatamuogopa na yuko tayari kuongea kuhusu hisia zake. Kwakuwa anajua anachokitaka atamuambia mwenza wake na kwakuwa ni marafiki basi kila mmoja atakuwa huru na mwenzake.
9. Mwanamke anayejitambua anajua kuwa mapenzi si maisha yake bali ni sehemu tu ya maisha yake, hawezi kusumbuliwa na mwanaume kwakua tu anapenda kwani anajua yuko imara vyakutosha kuvumilia upuuzi wa mwanaume yeyote. Ameiweka mbele furaha yaake kuliko ya watu wengine na anapoona hapati anachokitaka basi hujitoa mara moja kwenye aina hiyo ya mahusiano.
10. Mwanamke anayejitambua hawezi kupigania mwanaume kwani anafahamu kuwa mwanaume hachungwi na kama mwanaume anampenda basi hawezi kuhangaika hangaika na wengine. Anafahamu kuwa mwanaume anachepuka kwakuwa anataka na si sababu ya mwanamke mwingine hivyo basi humaliza mambo yake na mwanaume wake na hapotezi muda wake kugombana na mwanamke mwingine kwaajili ya mwanaume

Sunday, February 5, 2017

Madhara ya Kutumia Tishu kwa Wanawake-2

Madhara ya Kutumia Tishu kwa Wanawake-2      




Wiki iliyopita tulianza kujadili mada hii ya madhara ya kiafya ya kutumia tishu kwa mwanamke. Leo tunaendelea kuanzia tulipoishia:

Pia zipo tishu za kisasa ambazo huwa zinakuwa kwenye pakti maalum, zikiwa na kemikali kwa ajili ya kukata harufu na majimaji yenye pafyumu. Hizi huwa na madhara zaidi kwa sababu kemikali zilizopo kwenye tishu hizo, huwa na athari kubwa kwa afya ya viungo vya uzazi.

Matumizi ya tishu, huchangia kwa kiasi kikubwa ugonjwa wa Vaginosis, ambao husababisha mwanamke atokwe na uchafu kwenye sehemu zake za siri. Hii hutokea kwa sababu, katika njia ya haja kubwa, kuna bakteria ambao huwa hawana madhara kwa ajili ya kuulinda mfumo wa utoaji taka mwilini lakini bakteria hao wanapoingia kwenye viungo vya uzazi husababisha madhara.

Kwa kawaida, watumiaji wengi wa tishu, hujifuta kwa kutokea nyuma kuja mbele, jambo ambalo husababisha iwe rahisi kwa bakteria hao kuhamishwa kutoka njia ya haja kubwa mpaka kwenye mfumo wa uzazi na baadaye maambukizi hutokea.

Wataalamu wa afya, wanashauri kwamba, matumizi sahihi ya tishu, yanapaswa kuwa kama ifuatavyo:

-Hakikisha unanunua tishu zenye ubora uliothibitishwa, siku hizi umeibuka mchezo wa kutengeneza bidhaa feki ambazo hazina ubora unaotakiwa, zikiwemo tishu. Unaponunua tishu za kutumia, hakikisha unazingatia ubora na siyo bei.

-Badala ya kutumia tishu kujifuta (rub), unashauriwa kuzitumia kwa namna ya kama unachovya, kwa maana kwamba hujifuti kwa kusugua ngozi yako ili kuondoa hatari ya kupata michubuko.

– Epuka matumizi ya tishu zenye kemikali (wet diapers) au zenye manukato.

-Unapolazimika kutumia tishu kujisafisha (kama hakuna kabisa maji), lazima ujifute kwa mtindo wa kuanzia mbele kwenda nyuma, yaani, badala ya kuanzia kusafisha sehemu ya haja kubwa ndiyo uje kwenye viungo vya uzazi, anzia mbele kwenda nyuma. Hii itakusaidia kujikinga na kusambaza vijidudu vya magonjwa kutoka kwenye mfumo wa haja kubwa kwenda kwenye viungo vya uzazi.

Pendelea kutumia zaidi maji unapomaliza kujisaidia, iwe haja ndogo au kubwa na tishu zitumike kukausha unyevunyevu tu na siyo kuzitegemea kujisafishia kwa sababu hazina uwezo wa kuondoa uchafu wote bila kukusababishia madhara.

Friday, February 3, 2017

UNA MATATIZO YA KUSAHAU? SOMA HAPA

UNA MATATIZO YA KUSAHAU? SOMA HAPA

Kila seli katika mwili wa binadamu inahitaji kupata hewa ya oksijeni na virutubisho vya kutosha ili viungo vya mwili viweze kufanyakazi yake ipasavyo, zikiwemo seli za ubongo (Brain Cells).

Kwa kuwa hewa ya oksijeni na virutubisho hupita kwenye mfumo wa damu, kitu chochote kinachozuia upitaji huo wa damu husababisha seli kuathirika. Ni ukweli ulio wazi kwamba moyo unapokuwa na afya njema ndivyo ubongo nao unavyoweza kufanya kazi yake vizuri.

Ili ubongo wa mtu ufanye kazi vizuri, ni lazima hali ya moyo iwe nzuri pia. Hatua ya kwanza ya kuchukua ili kuwa na moyo wenye afya ni kujipima shinikizo lako la damu, kama haliko sawa, unatakiwa ulishughulikie tatizo hilo kwanza.
Zifuatazo ni hatua unazoweza kuchukua ili kujenga afya bora ya moyo wako na hatimaye ubongo kuwa na kumbukumbu nzuri:

PIMA SHINIKIZO
Pima hali ya shinikizo lako la damu pamoja na kiwango chako cha kolestro mwilini. Ubongo wenye afya unatokana na moyo wenye afya nzuri na vitu hivyo vinategemeana.

PATA MUDA WA KULALA
Pata muda wa kutosha kulala. Utafiti unaonesha kuwa kukosa muda wa kulala huathiri mfumo wa kumbukumbu ya ubongo.

FANYA MAZOEZI
Fanya mazoezi mara kwa mara. Mazoezi ya mara kwa mara yameonesha kupunguza uwezekano wa mtu kupatwa na magonjwa mbalimbali. Fanya mazoezi angalau kila siku kwa dakika 30 tu.

CHANGAMSHA UBONGO
Usiulaze ubongo wako, upe changamoto kwa kufikiri na kutatua mambo kadhaa ya kimaisha, kwa kufanya hivyo utauchangamsha.

USIVUTE SIGARA
Usivute sigara, kwa sababu uvutaji wa sigara huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa moyo na husababisha madhara makubwa iwapo damu itashindwa kwenda kwa wingi kwenye ubongo kama inavyotakiwa.

JIPUMZISHE
Pata muda wa kupumzisha akili kwa kutafuta njia za kuondoa msongo wa mawazo katika kichwa chako.

VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUONGEZA KUMBUKUMBU
Utafiti ulio angalia uhusiano kati ya kumbukumbu na vyakula, umeonesha kuwa kadri mtu anavyokula aina nyingi ya vyakula asili ndiyo uwezo wa kumbukumbu yake unavyoimarika.

Utafiti wa muda wa miaka 25 uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard nchini Marekani, uliowahusu zaidi ya watu 13,000, umeonesha kuwa watu waliokula kiasi kikubwa cha mboga mboga kwa miaka mingi, walikuwa na athari ndogo ya kupungukiwa na kumbukumbu baada ya kuzeeka.

Miongoni mwa mboga zenye kiasi kikubwa cha virutubisho vinavyoongeza kumbukumbu ni pamoja na Brokoli, kabichi na maua ya maboga. Zingine ni mboga za kijani kama vile mchicha, majani ya maboga, nk.

Kwa upande wa matunda, aina zote za ‘beri’, zabibu za rangi ya papo (Purple Grapes), tufaha nyekundu (Red Apples) na matunda yanayojulikana kama vitunguu vyekundu (Red Onions).

Halikadhalika vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Folic Acid, husaidia sana katika kuongeza kumbukumbu. Mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na nafaka zisizo kobolewa, maharagwe meusi, brokoli, ngano, machungwa, n.k.

SAMAKI
Watafiti wa Rush University Medical Centre, Chicago nchini Marekani, walifuatilia watu 3000, wake kwa waume, kwa muda wa miaka sita kuona ni kwa kiasi gani lishe huathiri kumbukumbu ya mtu.

Utafiti huo ulionesha kuwa watu waliokula samaki angalau mara moja kwa wiki, walionesha kupoteza kumbukumbu taratibu kwa asilimia 10 ukilinganisha na wasiokula samaki. Kiasi hicho kiliwapa uwezo wa kufikiri na kuwa na kumbukumbu sawa na kijana waliyemzidi umri wa miaka mitatu.

Thursday, February 2, 2017

KWA NINI MTOTO MCHANGA HATAKIWI KUPEWA MAJI

KWA NINI MTOTO MCHANGA HATAKIWI KUPEWA MAJI


Wakina mama wengi wanakuwa wanajiuliza bila kupata majibu kama ni sahihi kumpa mtoto mchanga maji .Taasisi za afya dunia kama (World health organization) hazishauri mtoto chini ya miezi 6 kunywa maji,sababu tafiti nyingi zimeonyesha kwamba maziwa ya mama au baby formula yanakiasi cha maji ya kutosha kumtosheleza mtoto.


Sababu zinazomfanya mtoto asipewe maji

Maji kuharibu uwezo wa mwili wa mtoto kunyonya virutubisho vya maziwa ya mama ipasavyo.Maji yatamjaza tumbo mtoto kumfanya ashibe na atashindwa kunyonya kwa kiasi kinachotakiwa.Water intoxication-hii ni hali ya mwili kuwa na kiwango kikubwa cha maji na kuadhiri afya ya mtoto anaweza akazimia mara kwa mara na kumpelekea hata kukaa comaMaji sio salama ,mwili wa mtoto bado ni mdogo hauna kinga ya kutosha kupigana bakteria au virus wanao weza patikana kwenye maji.

Mtoto anaweza pewa kiwango kidogo cha maji iwapo

Anaishi eneo lenye joto kali sana ,anaweza pewa vijiko 2-3 vidogo vya chaiMtoto alieanzishiwa kunywa uji mwepesi kabla ya miezi 6 anaweza pewa  vijiko 3-4 vya chai mara 2 kwa siku.



Ushauri
 afyaborakwamtotoWatoto wanaopewa maziwa ya kopo (baby formula) au maziwa ya mama hawana haja ya kupewa maji mpaka watakapo fikisha miezi 6,mama anaenyonyesha anatakiwa kunywa maji kwa wingi isipungue glasi 7-8 kwa siku.Mama anaweza kuzalisha maziwa machache na ikamfanya mtoto asishibe hivyo anaweza kupika uji mwepesi  iwapo mzazi  hana uwezo wa  kuwanunulia maziwa ya kopo ,mtoto anekunywa uji  apewe maji ya kunywa kwa kuzingatia vipimo sahihi vijiko 3-4 mara 2 kwa siku,ili kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

Wednesday, February 1, 2017

SIFA 6 ZA MWANAUME ANAYESTAHILI KUWA MUMEO!

SIFA 6 ZA MWANAUME ANAYESTAHILI KUWA MUMEO!


Wiki hii nitazungumzia sifa 6 za mwanaume ambaye anastahili kuwa mumeo. Nafanya hivi ikiwa ni msaada kwa wale ambao wamefikia hatua ya kuingia kwenye ndoa lakini bado wanashindwa kutambua yupi ni sahihi na yupi si sahihi kuitwa mume.

Tufahamu kwamba si kila mwanaume unayekutana naye na ukampenda anafaa kuwa mumeo. Wengine wana mapungufu makubwa ambayo bila kuyabaini na ukaingia kichwakichwa, utakutana na matatizo makubwa.

Kwa maana hiyo basi, sifa hizi sita ambazo nitazizungumzia leo endapo utaziona kwa huyo ambaye macho yako yameganda kwake, fanya maamuzi sahihi ya kumkubalia.

Anakupenda kwa maana ya kukupenda
Unapoingia kwenye maisha ya ndoa, unatarajia kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwenza wako. Wapo wanaume ambao wanaonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.

Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na demu flani bomba au kuonja tu penzi kisha kuanza visa ili muachane.Kwa nini ni vizuri kumpata mwanaume mwenye mapenzi ya dhati? Hii inatokana na ukweli kwamba kinyume na hivyo, maisha yatakuwa ya migogoro kila siku. Atakufanyia mambo ya kukuumiza kwa kukusaliti bila kujali maumivu utakayopata. Hii yote ni kwa sababu hana mapenzi ya kweli na wewe.

Ndiyo maana unashauriwa kwamba, kabla hata ya kumuonjesha penzi kisha kufanya maamuzi ya kumruhusu aende kwa wazazi wako ili mfunge pingu za maisha, ni vyema ukawa na uthibitisho kwamba anakupenda kwa moyo mmoja.

Hili la tabia ndo’ kila kitu

Linapokuja suala la ndoa, tabia inakuwa kitu cha awali sana kuangaliwa. Hii ni kwa sababu, wapo wanaume ‘handsome’, wenye kazi nzuri na kipato kizuri lakini wanakosa sifa ya kuitwa mume kutokana na tabia zao chafu.

Hakuna mwanamke anayeweza kudiriki kumpa nafasi mwanaume kuwa mume wake wakati ana tabia chafu. Endapo utaangalia uzuri wa sura kisha ukafanya maamuzi ya kuolewa naye, utakuwa umejichimbia kaburi.

Awe anaota mafanikio
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanawake. Wengi hawapendi kabisa kuolewa na mwanaume ambaye hana kazi.
Mwanaume anatakiwa kuwa dereva katika safari ya kusaka mafanikio, sasa kama atakuwa ni mtu wa kukaa kijiweni, kupiga mizinga, mvivu asiyependa kujishughulisha kwa namna yoyote, huyu hafai kupewa nafasi ya kuitwa mume.

Ile dhana ya kukubali kuolewa na mwanaume yoyote ili mradi upate heshima ya kwamba umeolewa, imepitwa na wakati. Mwanaume sahihi ni yule mwenye malengo maishani, anayefikiria nini cha kufanya kwa ajili ya maendeleo yake, mkewe na watoto wao.

Wa shida na raha
Wapo wanaume ambao siyo wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.

Kwa mfano, unaweza kuingia kwenye maisha ya ndoa lakini kwa bahati mbaya ukawa huna kizazi, mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na wewe anatakiwa kukuvumilia na kuwa upande wako.
Yule ambaye atakuwa anaungana na dada zake kukushambulia kwa kutozaa, hafai kuwa na wewe kwani yapo mengi yanayoweza kutokea yanayohitaji kuvumiliana.

Kimsingi uvumilivu kwa mwanaume utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.

Anayejua thamani ya mke
Wapo wanaume ambao hawajui thamani ya mke na ukiwachunguza utabaini hawafai kuwa waume za watu. Mume sahihi ni yule anayejua kwamba mke ni kitu cha faraja kwenye maisha yake.
Yule anayeamini kwamba, bila mke maisha yake hayawezi kuwa yamekamilika. Wapo ambao wanaamini hata bila wanawake wanaweza kuwa na maisha mazuri.

Mwanaume mwenye dhana hii, ukimpa nafasi kwenye moyo wako na ukaingia naye kwenye maisha ya ndoa, lazima atakuwa mguu ndani, mguu nje. Hataona hatari kukupa talaka hata kwa jambo dogo tu ambalo mnaweza kuongea na mkalimaliza.

Ndiyo maana nikasema, mwanaume sahihi wa kumpa nafasi ya kuwa mumeo ni yule anayejua thamani ya mke, anayeweza kuvumilia yote akijua mke ndiye anayekamilisha maisha yake.

Asiye na tamaa za kijinga
Unaweza kuwa na mpenzi wa kawaida ukiwa na malengo ya kumfanya awe mumeo katika siku za baadaye. Huyu ukigundua ana tamaa, huna sababu ya ‘kumpetipeti’.
Wanaume wenye tamaa za kijinga ndiyo ambao wakishaingia kwenye maisha ya ndoa wanakuwa wepesi kusaliti. Hao hawastahili kuitwa waume za watu.

Mwisho kabisa naomba niseme kwamba, licha ya sifa hizo 6, yapo mambo mengine ambayo ukiyaona kwa mwanaume ambaye ulikuwa unahisi anafaa kuwa mumeo, ni vyema ukapingana na mawazo.
Mwanaume asiyepitwa na sketi, asiyependa kumsikiliza mwenza wake, anayependa kufanya maamuzi bila kutaka kumshirikisha mwenza wake, anayekuwa upande wa ndugu zake unapokuwa kwenye matatizo, asiyejali familia yake, anayekuona wewe si lolote, asiyethamini na kuwaheshimu ndugu na marafiki zako, huyo kaa naye mbali kabisa.

Ni hayo kwa leo